RAIS DKT. MAGUFULI ATOA MAAGIZO WATUMISHI WOTE KUMALIZAKUJAZA FOMU ZA MAADILI KABLA YA TAREHE 30,DISEMBA,2020.

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA MAAGIZO WATUMISHI WOTE KUMALIZAKUJAZA FOMU ZA MAADILI KABLA YA TAREHE 30,DISEMBA,2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli  leo Disemba 24,2020 amemwapisha  kamishna wa Maadili  Jaji Sivangilwa Mwangesi huku akitoa maagizo kwa watumishi wote kuhakikisha  wanakamilisha kujaza fomu za maadili ya utumishi wa umma kabla ya tarehe 30,Disemba ,2020. Akizungumza mara baada ya uapisho huo uliofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma Rais

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli  leo Disemba 24,2020 amemwapisha  kamishna wa Maadili  Jaji Sivangilwa Mwangesi huku akitoa maagizo kwa watumishi wote kuhakikisha  wanakamilisha kujaza fomu za maadili ya utumishi wa umma kabla ya tarehe 30,Disemba ,2020.

Mhu. Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Akizungumza mara baada ya uapisho huo uliofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa ifikapo Disemba 30,2020 watumishi wote wahakikishe wanakamilisha kujaza fomu kabla ya Tarehe ,30,2020.

Aidha,Rais Dkt.Magufuli ametoa maagizo kwa tume ya Maadili kuacha kurudisha fomu kwa njia ya mtandao  ili kuepuka wahalifu wa mtandao wanaoweza kughushi na kuleta mtafaruko.

 Kamishna wa maadili     Sivangilwa Mwangesi ameahidi kutekeleza majukumu yote aliyopewa kwa kufuata miongozo ya nchi.

 Kamishna wa maadili Sivangilwa Mwangesi.

Akitoa Salam za pongezi,Naibu katibu mkuu Wizara ya katiba ba Sheria Amon Mpanju ameomba mhimili wa Mahakama kuongezewa nguvu  kwa kuongeza majaji  huku Naibu Waziri wa Menejimenti  ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi  amebainisha kuwa  mpaka sasa karibia asilimia 92 ya watumishi wa umma wanajaza fomu za utumishi wa umma na kutaja mali zao.

 

Ikumbukwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani Sivangilwa Mwangesi kuwa Kamishna wa Maadili kuanzia  Tarehe 23 Disemba 2020 ambapo  Jaji Mwangesi anachukua nafasi ya Marehemu Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Harold Nsekela aliyefariki Dunia hivi Karibuni.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »